Muhtasari wa Dayosisi ya Iringa

Jimbo Katoliki la Iringa ni mojawapo ya Jimbo Katoliki Tanzania eneo la Nyanda za Juu Kusini.  Mkoa una ukubwa wa kilometa za mraba zipatazo 29,000,000. Jimbo letu lina  Manispaa ya Iringa, Wilaya ya Iringa vijijini na wilaya ya Kilolo. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, dayosisi yetu ina wakazi wapatao 463,000 waishio humo. Askofu wa Jimbo letu ni Tarcisius Ngalalekumtwa ambaye ni mzaliwa wa Jimbo hili kutoka Parokia ya Tosamaganga, Jimbo letu lina idadi ya parokia 34 na Vikaria 7

Kuboresha ustawi wa idadi ya watu

Maono yetu ni kufanya kazi za kidini na kichungaji kwa ajili ya ustawi wa kiroho wa wakazi wa Jimbo la Iringa. Dhamira yetu ni kusaidia katika kukuza manufaa ya wote kwa watu wanaoishi ndani ya jimbo la Iringa bila kujali imani. Tunajali ustawi wao wa kiroho na kijamii pia.

Dayosisi yetu kuna idara mbalimbali zinazopatikana. Idara ni pamoja na elimu, mawasiliano, walei. Pia tuna ofisi yetu ya utawala ambayo inajishughulisha na masuala mbalimbali ya watumishi lakini pia na utoaji wa vibali kwa wageni wanaotoka nje ya nchi ambayo inatoa taarifa kuhusu dayosisi yetu. Katika ofisi ya utawala unaweza kupata taarifa zote kuhusu dayosisi.

 

Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu

Kanisa kuu la dayosisi hiyo lipo Iringa kilomita chache kutoka katikati ya jiji eneo la Kihesa.