ASKOFU TARCISIUS NGALALEKUMTWA
Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, ni askofu wa Iringa tangu Novemba 1992 ni askofu anayependa sana elimu na ndiye aliyeanzisha kituo cha vijana cha Kichangani ambapo vijana wanakuja kujisomea.
Pia anapendelea kilimo na ndiye aliyeanzisha kilimo hicho shambani eneo la “Igang’idumu” kwa matumizi ya chakula katika eneo analoishi lakini pia kwa wale wanaohitaji chakula.
Kauli mbiu yake ni “Uweza watoka Juu”.

HISTORIA FUPI YA ASKOFU NGALALEKUMTWA
Askofu Ngalalekumtwa ni mtoto wa Joseph Msengidunda Ngalalekumtwa na mama yake ni Magdalena Sekutika. Alizaliwa Tosamaganga
Mwaka 1954, alianza masomo katika shule ya msingi (Lower school) Tosamaganga. Mwaka 1960, alitumwa na paroko wake katika seminari ya Tosamaganga.
Wito wake wa ukuhani ulianza zamani alipokuwa mdogo. Alihitimu masomo yake ya seminari mwaka 1963 na baada ya hapo alipelekwa kusoma zaidi nchini Italia.
Utaratibu wa kitakatifu wa ukuhani. Alitawazwa tarehe o7/o4/1973 nchini Italia. Amefanya utume wake katika Jimbo la Iringa kama Paroko wa Parokia ya Ifunda na Gambera ya Seminari ndogo ya Mafinga. Kwa miaka kadhaa amefanya misheni yake katika seminari ya Paramiho Kuu kama mwalimu, mlezi na gambera.
Kuteuliwa kuwa askofu. Mwaka 1989 aliteuliwa kuwa askofu mkuu wa jimbo katoliki la Sumbawanga. Alitangazwa kuwa askofu wa nne wa Jimbo Katoliki la Iringa Novemba 21, 1992. Askofu Ngalalekumtwa aliadhimisha miaka 50 ya upadri wake mwaka 2023. Amekuwa askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa kwa miaka 30.