Makamu wa Askofu Pd. Paulo Msombe

Pd. Paulo Msombe ni Makamu wa Askofu Jimbo Katoliki la Iringa. Pamoja na majukumu ya kitume aliyonayo, ni msaidizi wa askofu katika masuala mbalimbali ya kichungaji ndani na nje ya jimbo .
Moja ya shughuli za kichungaji ni kutoa sakramenti ya kipaimara au kumwakilisha askofu katika mikutano pale anapopasika.
Kulingana na (C.I.C. 475)- “Askofu kwa yeye mwenyewe anazo nguvu za kisheria katika kutekeleza wajibu wake. Anatekeleza majukumu yake au yeye mwenyewe au njia ya makamu wake. Anatekeleza majukumu yake au yeye mwenyewe au kwa njia ya makamu wake au washiriki wa Askofu kwa kadiri ya sheria. Makamu wa Askofu anateuliwa na askofu ili kumsaidia katika shughuli nzima ya kulitawala jimbo”. Makamu wa Askofu anazo nguvu za kiutawa.

Pd. Paulo Msombe alizaliwa katika Parokia ya Wasa na kusoma katika Seminari ya Peramiho iliyopo Jimbo kuu la Songea. Amesimikwa katika Parokia ya Wasa tarehe 06/07/1994, pia ni Paroko wa Parokia ya Tosamaganga